Sunday, March 5, 2017

Michael Owen na Martin Keown waipa ushindi Tottenham


Michael Owen na Martin Keown waweka hadharani utabiri wao Tottenham vs Everton
Mchezaji wa zamani wa Manchester United  Michael Owen ameitabiria ushindi  tottenham dhidi ya Everton katika dimba la White Hart Lane.

Owen alisema “namwaangalia Harry Kane na Romelu Lukaku  naona magoli kutoka kwao lakini mwenyeji atashinda mchezo huu”

Utabiri wa Owen ni kuwa timu zote zitapata magoli lakini Tottenham watashinda mchezo huo. Owen aliandika kwenye Betvictor.com.

Kwa upande wa mchezaji wa dhamani wa arsenal Martin Keown alikaririwa na gazeti la Daily Mail akizungumzia mchezo wa leo kwa kusema “Tottenham wapo vizuri na kuwa nyumbani kutawaongezea nguvu”.


“si kazi ndogo kuishinda Everton lakini nasema Matokeo yatakuwa 2 - 1”.

0 comments:

Post a Comment