mchezo wa mapema wa kombe la FA umemalizika kwa matokeo ambayo liverpool watayakumbuka sana.
Ikiwa ndani ya dimba la anfield majogoo wa jiji wamekubali
kipigo cha magoli 2 – 1 kutoka kwa Wolverhampton Wanderers .
Iliwachukua dakika moja tu baada ya kuanza kwa mchezo kwa Wolverhampton
Wanderers kujipatia goli la kuongoza
kupitia kwa Richard Stearman.
Mchezo uliendelea kuwa
wa vuta ni kuvute na ukishuhudia kadi nne za njano tatu kwa wageni Wolverhampton Wanderers na moja kwa Liverpool.
Liverpool wakiwa wanatafakari kuchomoa goli hilo moja mnamo
dakika ya 41 Andreas Weimann aliongeza maumivu kwa goli zuri na kuipa timu yake
uongozi wa goli 2 – 0 mpka mapumziko.
Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko kwa upande wa
Liverpool waliwatoa Connor Randal 46’ nafasi yake kuchukuliwa na Philippe
Coutinho, wakamtoa tena Roberto Firmino 65’ nafasi yake kuchukuliwa na Daniel
Sturridge, na walihitimisha kwa kumtoa Ovie Ejaria 74, na kumuingiza Emre Can.
Kwa upande wa Wolverhampton Wanderers wao pia walifanya
mabadiliko matatu kwa kuwatoa Helder Costa 67’ na kuingia Connor Ronan, ilimtoa
tena Nouha Dicko 70’ nakuingia Jon Dadi Boedvarsson, ilihitimisha kwa
kumtoa Andreas Weimann 77’ na kuingia Joe
Mason.
Mabadiliko hayo yaliisadia Liverpool kupata goli la kufutia
machozi mnamo dakika ya 86 kupitia Orig
FT Liverpool 1 – 2 Wolverhampton Wanderers
0 comments:
Post a Comment