Sunday, January 29, 2017

Bossou Kucheza Dhidi Ya Mwadui Leo Taifa?

Beki kisiki wa Yanga, Vicent Bossou anatarajia kurejea nchini Leo Jumapili akitokea nchini kwao Togo baada ya kukosekana kwa muda wa mwezi mmoja alipokuwa akiitumikia timu yake ya taifa huko nchini Gabon katika michuano ya AFCON.

Baraka Deusdedit amesema Bossou amewahakikishia Yanga kuwa Jumapili hii atakuwa amewasili kambini tayari kwa kuitumikia klabu yake ya Dar Young Africans.

“Tumeongea na mchezaji na ametuhakikishia hadi Jumapili atakuwa aewasili kambini kwasababu timu inamuhitaji kutokana na mikakati tuliyokuwa hivyo tunamuombea mungu ili aweze kurejea salama,”amesema Baraka.

Togo, imeondolewa katika michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika katika hatua ya makundi baada ya kuambulia pointi moja tu katika mechi zao tatu walizocheza katika hatua ya makundi, ilichapwa 3-1 na Congo DR, ikaja kuchapwa tena 3-1 dhidi ya Morocco kabla hawajatoa suluhu dhidi ya Ivory Coast.

0 comments:

Post a Comment