Ubishi kumalizwa Camp Nou siku ya jumamosi wakati miamba
miwili ya soka Barcelona na Real Madrid watakapoonyesha kazi katika mchezo
muhimu wa ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama ‘LaLiga Santander’
Tukiiangalia Barcelona, kwa msimu huu ni kama mambo yanawaendea
vibaya hawawapi raha mashabiki wao kama walivyozoea, kiufundi baada ya beki wao
kisiki Gerard Pique Kuwa na maumivu ya ankle na kucheza chini ya kiwango kwa
muagentina Javier Mascherano huenda kukamlazimu kocha Luis Enrique kocha wa Barcelona
kumuanzisha Samuel Umtiti ambae katoka kwenye majeruhi. Chakufurahisha kwa Barcelona ni kupona kwa Iniesta
na Alba hivyo kutaongeza morali kwa wachezaji.
Kwa upande mwingine kocha zidane atakuwa katika wakati mgumu
pale atakapowakosa wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza Toni Kroos na
Gareth Bale hivyo ambapo inatabiriwa huenda akabadili mfumo wa uchezaji kutoka
4 -3 -3 kwenda 4 -2 -3 -1 akiwatumia Casemiro , Mateo Kovacic na Luka Modric
eneo la katikati.
Zidane alipohojiwa na vyombo vya habari alisema yeye
anasubiri dakika 90 wakati
Takwimu kwa timu zote mbili kuelekea mchezo huo zinaibeba
real Madrid kuibuka na ushindi na kukaribia kuikuta rekodi ya 1988/89 ya
kucheza michezo 34 bila kupoteza mpka sasa Madrid imecheza michezo 31 bila
kupoteza
Nani kuibuka mbabe tusubiri dakika 90 katika dimba la nou
camp kesho jumamosi kuanzia saa 18:15
Kombe Real Madrid vs matokeo
Copa Cultural L. 6-1 home
laLiga Sporting Gijon 2-1 home
Champions Sporting Portugal 1-2 away
laLiga Atlético-madrid 0-3 away
laLiga Leganés 3-0 home
kombe Barcelona vs matokeo
Copa Hércules 1-1 away
Liga R. Sociedad 1-1 away
Champions Celtic Glasgow 0-2 away
Liga Málaga 0-0 home
Liga Sevilla 1-2 home
michezo mingine ya laliga kesho decemba 3 ni kama ifuatavyo:
Granada vs Sevilla 15:00
Leganes vs Villarreal 20:30
Atletico Madrid vs Espanyol 22:45
0 comments:
Post a Comment