Baada ya Shirikisho la miguu Tanzania TFF kukata rufaa juu
ya kijeba wa Congo-Brazzaville, Langa-Lesse Bercy na kufanikiwa kukidhi
mashariti yote ya CAF hatimae kijeba huyo ashindwa kuonekana.
CAF ilipanga 19 novemba kijeba huyo afanyiwe vipimo vya MRI
lakini taarifa zilizotolewa na CAF ni kuwa alishindwa kufanya hivyo.
Msemaji wa TFF akihijiwa na vyombo mbalimbali vya habari
hapa Tanzania juzi alisema “Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF
kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika
eneo lililoko "vitani",aliongeza kwa kusema “sisi TFF tumetitimiza
masharti yote tuliyopewa ikiwa ni Pamoja na kugharamia rufaa yote nauli ya
mchezaji huyo na daktari wake” sisi tunasubiri taarifa toka CAF.
Langa-Lesse Bercy alikua akafanyiwe kipimo chaMagnetic Imaging
Resonance (MRI) ili kutambua umri halisi wa mchezaji huyo.
Ikibainika kama amedanganya umri Serengeti Boys watafuzu
mojamoja michuano ya Mataifa Afrika na watakuwa kundi B Pamoja na Mali, Angola
and Niger hivyo kufungua milango kwa soka la Tanzania kimataifa. Na Congo
watapata adhabu ya kufungiwa kushiriki mahindano hayo kwa miaka mitatu.
Kwa hali ilivyo tunaamini Serengeti Boys watafanikiwa
kushiriki mashindano hayo, Serengeti ambao walikuwa na mwaliko huko korea
wanaendelea kujifua huku wakiomba dua mambo yawaendee kombo Congo
Langa-Lesse Bercy
0 comments:
Post a Comment