Katika mechi ya robo fainali kati ya Ureno na Poland shabiki mmoja wa Ureno aliingia uwanjani na kumkumbatia Christiano Ronaldo kabla ya kutolewa nje na wanausalama uwanjani hapo.
Shamshir Karimi 22, amezuiwa pia kuingia Ufaransa mwezi ujao.
Akitoa utetezi wake mahakamani shabiki huyo alisema alivamia uwanjani hapo kwa kuwa anamapenzi makubwa na Ronaldo.
Tukio hilo lilitokea katika dakikaya 110 ya mchezo na hiyo si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwa mashabiki kutaka kukutana na Ronaldo wakati mchezo unaendelea.
Shabiki mwingine alivamia uwanjani na kwenda kwa Ronaldo katika mchezo kati ya Ureno na Austria na kwa bahati nzuri lengo lake lilitimia baada ya kukubaliwa kupiga picha ya pamoja na Ronaldo.
0 comments:
Post a Comment