Ubora wa Guardiola umedhihirika akiwa na vilabu vya Barcelona na Bayern Munich lakini kwa sasa anakumbana na changamoto kubwa ya kuifanya klabu tajari duniani kutimiza malengo yake.
Soka24 inakuletea changamoto 6 ambazo Guardiola anakumbana nazo katika klabu yake mpya ya Manchester City.
1. Kuifanya Manchester Kuwa Wafalme Wa Soka Uingereza
Roberto Mancini na Manuel Pellegrini wote waliweza kuifanya City kuwa klabu tishio Uingereza, na sasa kazi imebaki kwa Guardiola hasa kutokana na rekodi zake katika klabu alizofundisha akionekana kuwa ni mmoja kati ya makocha bora duniani.
Changamoto hii inakuja kufuatia kauli ya mjumbe wa bodi ya klabu hiyo pale aliposema "Malengo yetu na Pep ni kushinda ligi kuu kila mwaka na kuifikisha timu yetu mbali zaidi katika michuano ya klabu bingwa kabla ya kulitwaa taji hilo moja kwa moja".
2. Kutwaa Ubingwa Wa Ligi Ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League)
Licha ya kushindwa kutwaa taji hilo akiwa na klabu ya Bayern Munich, Guardiola anaonekana kuwa ni tumaini jipya kwa klabu ya Manchester City katika ndoto zao za kutwaa ubingwa wa Uefa Champions, Guardiola alifanikiwa kubeba taji hilo mara mbili akiwa na klabu ya Barcelona. Kwa mara ya kwanza mwaka Jana Man City iliweza kutinga katika hatua ya mtoano katika michuano hiyo, hivyo watatamani kuona timu yao inavuka zaidi ya hapo.
3. Kuanzisha Staili Mpya Klabuni Hapo.
Guardiola ameonekana kubadilika katika mifumo yake ya ufundishaji, wakati akiwa Barcelona alikuwa anatumia mfumo wa umilikaji mpira, lakini akiwa na Bayern aliweza kupata njia zingine zilizomuwezesha kushinda mataji lakini bado akiwa anatumia falsafa yake ileile, Changamoto yake ni kutafuta mbinu mpya ambayo itaendana na mifumo yake huku pia ikileta mafanikio katika ligi ya Uingereza.
4. Kutatua Tatizo La Ulinzi
Licha ya kuwategemea sana walinzi Nicolas Otamendi na Eliaquim Mangala katika misimu miwili iliyopita, Manchester City inatatizo kubwa katika safu ya ulinzi. Ingawa Aymeric Laporte na John Stones wanahusishwa kujiunga na Man City, mfumo mpya unahitajika kuimarisha safu hiyo, na hili linaweza kuwa tatizo kubwa kwa Guardiola aliyefanya vizuri katika safu yake ya ulinzi akiwa na Bayern Munich.
5.Kusajili Wachezaji Wapya
Tayari Nolito na Gundogan wameshasaini Man City,Manchester city ya Guardiola inatakiwa iwe ya aina yake, huku tetesi zikisema kuwa City itakuwa na kikosi hatari licha ya Guardiola mwenyewe kukiri kuwa kuipata saini ya staa wa Barcelona Lionel Messi ni suala ambalo haliwezekani.
6. Jose Mourinho
Macho ya wapenda soka duniani msimu ujao yatakuwa katika vilabu vya Manchester, huku Guardiola na Mourinho wanakutana tena kuendeleza upinzani wao waliokuwa nao Hispania katika vilabu vya Barcelona na Real Madrid.
Mourinho atakuwa ni changamoto kubwa zaidi kwa Guardiola, hivyo kutakiwa kutafuta mbini sahihi za kukabiliana na kocha huyo mwenye maneno mengi.
0 comments:
Post a Comment