Tuesday, July 5, 2016

FIFA YAKATAZA WACHEZAJI KUSHEREHEKEA NA FAMILIA ZAO UWANJANI

Fifa inapanga kuzuia kitendo cha wachezaji kusherehekea ushindi na familia zao uwanjani katika michuano ya Euro inayoendelea huko nchini Ufaransa.

Mkurugenzi wa mashindano hayo Martin Kallen amesema zuio hilo ni kutokana na sababu za kiusalama.

"Hatupingi suala hili moja kwa moja, bali tunatakiwa kuchukua tahadhari na kuhakikisha usalama" alisema Kallen.

"Ni mashindano ya Ulaya na sio ya sherehe za kifamilia, uwanjani sio sehemu salama kwa watoto wadogo,watu wenye vibali maalumu tu ndo wataruhusiwa kuingia uwanjani na sio mtu mwingine yoyote " aliongeza Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia uwanja wa Stade de France ambao ndio utachezwa fainali ya michuano hiyo, Kallen alisema kila kitu kiko sawa na uwanja upo tayari kwa fainali hiyo.

"Hakutakuwa na tatizo lolote na kwa mechi zilizochezwa hivi karibuni tumeona kwamba uwanja wa Stade de France unaubora mzuri sana" alisema Kallen

Aidha Mkurugenzi huyo alilitolea ufafanuzi suala la timu kuzuiwa kufanya mazoezi katika viwanja vinavyochezwa baadhi ya mechi Kallen alisisitiza kwamba kulikuwa na suala la nyasi kutumiwa sana na ndio sababu iliyopelekea kuweka katazo hilo.

Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment