Tuesday, May 10, 2016

TFF YAZIKUMBUSHA TENA KLABU ZA LIGI KUU 2016/17

Kwa mara nyingine, Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka (TFF) imezikumbusha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kuwa mchakato wa wa utengenezaji kanuni umeanza tangu Mei 5, 2016.
Bodi ya Ligi kwa sasa inakaribisha maoni, mapendekezo, marekebisho kutoka klabu ili kuboresha uendeshaji wa ligi. Maoni hayo yanapokelewa kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za bodi au kwa njia ya barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.. Mwisho wa kupokea maoni hayo ni Mei 19, 2016.

0 comments:

Post a Comment