Manchester United Jana ilijikuta katika wakati Mgumu baada ya kuchezea kichapo cha jumla ya magoli matatu kwa bila kutoka kwa Tottenham. Man U ambayo kwa sasa kiwango chake kinatiliwa shaka na mashabiki na wapenzi wa mpira duniani kote iliruhusu kichapo hicho chini ya kocha wake Louis Van GaalMagoli ya Tottenham yalipatikana katika dakika za 70, 74 na 76 wafungaji wakiwa ni B. Alli, Lamela na Aldeweireld.
Matokeo hayo yanaiweka Manchester United katika nafasi ya 5 ikiwa imejikusanyia point 53, pointi 12 mbele ya Tottenham wanaoshika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi 65. Van Gaal bado anakuwa katika wakati mgumu huku tetesi zikimhusisha Jose Mourinho kwenda kuchukua nafasi yake kutokana na kiwango kibovu kinachoonyeshwa na kikosi cha Manchester United kwa sasa.
.
0 comments:
Post a Comment