Monday, April 11, 2016

Afisa Habari Wa Simba Anusurika Kifo


Afisa Habari wa Simba Sports Club Haji Manara amenusurika kifo jana kutokana na ajali ya bajaji, Manara alikuwa kwenye bajaji kwa bahati mbaya akachomoka kutokea nje wakati bajaji ikiwa kwenye mwendo mkali.
Ajali hiyo imemsababishia Msemaji huyo wa Wekundu wa Msimbazi majeraha katika sehemu zake za mkono na usoni.
“Nilikuwa nakwenda kumuona shangazi yangu, nikaamua kuacha gari nichukue Bajaj. Sasa tukio hilo limetokea hivi; Bajaj ilipiga tuta wakati nikiwa sijashika, ndiyo nikachomoka.

“Hakika nimeumia na nina maumivu makubwa sana, lakini namshukuru Mungu kwa kuwa ilikuwa ni ajali mbaya sana hasa kama kungekuwa na gari nyuma.

SOKA24 INATOA POLE KWA HAJI MANARA NA KWA WAPENZI WOTE WA SOKA

0 comments:

Post a Comment