Sunday, April 10, 2016

Farid Na Messi Waikalisha Esperance De Tunis

Azam fc imefanikiwa kuichapa timu ya Esperance kutoka nchini Tunisia kwa mabao mawili kwa moja. Esperance walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 33 ya mchezo kupitia kwa mchezaji wake Haithem Jouini.
Hadi timu zinakwenda mapumziko Azam walikuwa nyuma kwa bao moja.
Lakini goli hilo la Esperance halikuchukua muda baada ya Farid kuisawazishia Azam Fc dakika ya 68 baada ya kutanguliziwa pasi na Ramadhan Singano, dakika ya 70 dakika mbili tu baada ya Farid kuisawazishia Azam, Ramadhan Singano alitupia goli la pili naye akisetiwa vizuri na Farid Mussa.
Ushindi huu wa Azam unaiweka katika mazingira mazuri katika mchezo wao marudiano utakaofanyika majuma mawili yajayo.

0 comments:

Post a Comment