Tuesday, April 19, 2016

Christiano Ronaldo Kutua PSG



France football imetoa habari iliyotikisa zaidi kwa wapenzi wa soka ikimhusisha Star wa Real Madrid Christiano Ronaldo kutua katika klabu ya PSG.

Habari kutoka chanzo hicho zinaripoti kuwa Ronaldo amekutana mara 5 na Rais wa klabu ya PSG Nasser Al-Khelaifi. Habari zaidi zinasema mara ya mwisho kukutana kwa watu hao wawili ilikuwa ni wiki moja iliyopita.
Hii inatoa picha ya wazi kuwa PSG wanamhitaji Ronaldo.

Ronaldo na Maria Borges
Ronaldo pia akiwa Paris alipata kula chakula cha jioni na Mwanamitindo Maria Borges , Wawili hao walikutana mara baada ya Ronaldo kufunga Hat-trick dhidi ya Wolfsburg.

Habari zinaeleza kuwa Ronaldo alitumia ndege ya binafsi alipoenda kukutana na Rais huyo wa PSG na alirudi asubuhi ya siku iliyofuata.

0 comments:

Post a Comment