Siku ya jumamosi novemba 19 wapenda soka wa hispania na
dunia kwa ujumla watasimama kwa muda wa dakika 90 kupisha mtanange
unaaosubiriwa kwa hamu na na wapenzi wa soka ulimwenguni wakati Atletico Madrid
watakapo wakaribisha mahasimu wao wa mji mmoja Real Madrid.
Vijana wa Diego Simeone wanaikaribisha Real Madrid ambayo
mpka sasa imecheza michezo 28 bila kupoteza hata mmoja na wakiwa katika
harakati za kuvunja rekodi ya 1988/89 walipocheza michezo 34 bila kupoteza.
Mchezo huo utakaofanyika katika dimba la Estadio de
Mendizorroza unatizamwa na Atletico Madrid kama mchezo wa kulipa kisasa baada
ya kupoteza mchezo wake uliopita kwa kukubali kichapo cha 2 – 0 kutoka kwa Real
Sociedad.
Real Madrid ambayo ipo mbele ya Atletico Madrid kwa point 6
inahitaji alama tat umuhimu ili iendelee kujitawala vizuri ikumbukwe kuwa real
Madrid ipo mbele ya Barcelona kwa point 2.
Historia inatuambia kua Madrid derby imepigwa mara 55 huku
Real Madrid wakishinda mara 32 na Atletico Madrid wameshinda mara 14 na kutoka
sare michezo 9.
Katika michezo 6 iliyopita miamba hiyo imegawana ushindi
sawa, namainisha Real na Atletico zote zimeshinda 2 na kutoka sare 2.
Nani ataibuka mshindi mimi na wewe tutabashiri ila ukweli ni
kipyenga cha mwamuzi baada ya dakika 90.
0 comments:
Post a Comment