Friday, July 1, 2016

JAMES RODRIGUEZ AITAJA KLABU ANAYOTAKA KUHAMIA

James Rodriguez amesema anataka kujiunga na wababe wa soka la Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain msimu ujao.

Rodriguez alikuwa akihusishwa sana kutimkia ligi kuu ya Uingereza lakini amesema anatamani kujiunga na PSG.

Mkolombia huyo amekuwa akitumikia muda wake mwingi benchi katika klabu yake ya Madrid chini ya kocha Zidane hivyo kutaka kutimka klabuni hapo na kwenda kujaribu kwingine.
Kwa mujibu wa Mirror, Rodriguez amewashiwa taa za njano klabuni hapo na anaweza kujiunga na klabuu yoyote apendayo.

Kuwasili kwa Jose Mourinho Manchester United kulipelekea baadhi ya watu kumuhusisha Rodriguez kujiunga na mashetani wekundu huku pia klabu za Manchester City na Chelsea zikionyesha kuhitaji huduma ya Winga huyo.

Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment