Monday, July 11, 2016

CANNAVARO AIPANIA MEDEAMA

Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" amesema Ushindi kwenye mechi dhidi ya Medeama ni lazima.

Yanga inashiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC) hatua ya makundi na tayari imeshacheza mechi 2 na kupoteza michezo hiyo yote.

Nahodha wa klabu hiyo Nadir Haroub amesema watapambana kadri wawezavyo ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

Yanga kwa sasa ipo katika mazoezi makali chini ya kocha Hans Van Pluijm kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Medeama mchezo ambao utatoa taswira halisi ya muelekeo wa Yanga katika michuano hiyo.

"Tunataka kufanya vizuri, kila mchezaji anataka kushinda, Usidhani wachezaji wanafurahia hali ya kupoteza, Hivyo tunaendelea na mazoezi kwa juhudi zote. Tunataka kushinda dhidi ya Medeama ili kufufua matumaini" alisema nahodha huyo.

Yanga inatakiwa kushinda katika mchezo huo ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali kwani kwa sasa wanashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa Group A, baada ya TP Mazembe, MO Bejaia na Medeama.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment