Wednesday, May 18, 2016

MKWASA ATAJA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA



Kocha Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 27 watakaounda Taifa Stars ambacho kinajiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017).

Mkwasa maarufu kama Master, alitangaza kikosi cha timu hiyo leo Mei 18, 2016 mbele ya Kocha Msaidizi, Hemed Morocco na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuiva Misri, kikosi hicho kitafunga safari hadi Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao wenyeji wameuombea Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwamba utambulike na kuingia kwenye rekodi za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye mchakato wa kupima viwango vya soka.

Katika kikosi hicho, Mkwasa amemuita beki Mlinzi mahiri wa Young Africans, Nadir Haroub maarufu kama Cannavaro huku akimwacha beki mwingine wa Young Africans, Kelvin Yondani kwa sababu ya sentahafu huyo anatumikia kadi mbili za njano alizoonywa katika michezo iliyopita.

“Yondani ana kadi mbili za njano,” amesema Mkwasa ambako katika kikosi chake amewateua makipa, Deogratius Munishi (Young Africans), Aishi Manula (Azam FC) na Benny Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati mabeki ni Horoub, Mwinti Haji na Juma Abdul (Young Africans), Aggrey Moris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Mbwana Samatta (KDC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Young Africans) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

Related Posts:

  • Yanga Kufanya Uchaguzi Tarehe Hii Hapa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo imetangaza Juni 05, 2016 kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi ndani ya klabu ya Young Africans SC ya jijini Dar es salaam. Akiongea na waandishi … Read More
  • Azam FC Yatinga Fainali Kombe La FA Azam Fc imetinga hatua ya fainali ya kombe la shirikisho baada  ya kuiondosha Mwadui Fc kwa mikwaju ya penati 5-3. Mechi hiyo ambayo ilikuwa na kasi na ushindani mkubwa ilimalizika kwa sare ya 1 - 1 katika dakika 90… Read More
  • Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi Ya Coastal Union NUSU FAINALI  KOMBE LA SHIRIKISHO (FA CUP). Coastal Union SC Vs Young African SC. Uwanja- Mkwakwani KIKOSI CHA YANGA LEO. Deogratius Bonaventura Munish Juma Abdul Japhary Oscar Fanuel Joshua Nadir Haroub Canna… Read More
  • Farid Mussa Aanza Majaribio La Liga WINGA machachari wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, ameanza majaribio rasmi nchini Hispania akiwa na kikosi cha timu ya CD Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo. Farid,… Read More
  • BREAKING NEWS: Mechi Kati Ya Coastal Na Yanga Yavunjika Mechi kati ya Coastal na Yanga imevunjika baada ya vurugu zilizoanzishwa na mashabiki wa Coastal Union Baada ya Yanga kuongeza goli la pili katika dakika 30 za nyongeza goli lililofungwa na Hamisi Tambwe dakika ya 100 ya… Read More

0 comments:

Post a Comment