Saturday, May 21, 2016

MBAO FC YAAHIDI MAKUBWA LIGI KUU

Timu ya Mbao FC iliyopanda daraja Kufuatia maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya TFF ya kuzishusha daraja timu 4 za kundi C na kuifanya Mbao kushika nafasi ya kwanza katika kundi hilo..Imeahidi kuwashangaza wapenda soka katika ligi kuu Tanzania Msimu ujao.




Mbao FC ya jijjini Mwanza itashiriki ligi kuu msimu ujao na tayari viongozi na mashabiki wa timu hiyo wameanza vita ya maneno na vilabu vitakavyoshiriki ligi kuu msimu wa 2016/17, wakizungumzia hatua ya timu yao kushiriki Ligi kuu mashabiki na viongozi wa klabu hiyo wametamba kwa kusema watafanya makubwa katika ligi hiyo yatakayomshangaza kila mtu.

Mwenyekiti wa klabu hiyo amesema hatua hiyo ni nzuri kwao na watajitahidi kukusanya pesa kutoka kwa wadau mbalimbali ili kukisuka vizuri kikosi chao kiweze kuleta ushindani mkubwa katika ligi.

"Utakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Mwanza, kwa sasa Mwanza itakuwa na timu ambayo ni Neutral (isiyoegemea upande wowote) haina cha kumpa mtu pointi, hakuna cha kusema huyu ni mwenyeji wa hapa ashinde na huyu afungwe, tumerudisha furaha ya mpira wa Mwanza" alisema Danny aliyejitambulisha kuwa ni mwanachama wa Mbao FC.

Mbao Fc ni timu ambayo ilianzishwa na wafanyabiasha wa biashara ya Mbao kama ilivyo kwa Stand United iliyoanzishwa na Wapiga debe wa Stand.

Kila La Kheri Mbao FC katika safari yenu Kuelekea Ligi kuu Bara.

Related Posts:

  • Simba Nayo Sasa Ni Ya Kimataifa Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 20… Read More
  • TFF Yatuma Salamu Za Rambirambi MZFA Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa FAT Silvanus Maka… Read More
  • Misri Waihofia Stars AFCON Timu ya taifa ya Misri katika kile kinachoonekana kupania kuiondoa Taifa Stars katika michuano ya kufuzu mashindano ya Afcon 2017, wapo nchini kuifuatilia Stars kila hatua. Taarifa zinasema Meneja wa Timu hiyo yupo nchi… Read More
  • Azam Fc Kuifuata Esperance De Tunis KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kuondoka leo kuelekea jijini Tunis kwa ajili ya kukabiliana na Esperance ya huko kwenye mchezo wa marudiano wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika utaka… Read More
  • Hiki Ndio Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi Ya Mtibwa Sugar LIGI KUU || TZ - BARA || 2015~2016. YANGA SC Vs MTIBWA SUGAR FC. UWANJA - Uwanja wa Taifa. Muda - saa 10 : 00Alasiri. >>>>>>KIKOSI CHA YANGA LEO<<<<<<<< 1. Deogratias Bonave… Read More

0 comments:

Post a Comment