Monday, April 18, 2016

Yanga Yapata Dawa Ya Al Ahly




Mabingwa wa Tanzania mara 25 Young Africans imeondoka jumapili hii kuelekea nchini Misri kuvaana na wababe wa soka Afrika Timu ya Al Ahly Jumatano hii katika mchezo wa marudiano Klabu Bingwa Afrika hatua ya 18 bora. Yanga inaondoka ikiwa inajiamini kuwa itapata matokea mazuri dhidi ya mabingwa mara 8 wa michuano hiyo timu ya Al Ahly.

Katika mchezo wa kwanza Yanga walisawazisha kufuatia Al Ahly kufunga goli katika dakika za mapema kabisa za mchezo uliofanyika Jijini Dar Es Salaam.
Kocha mkuu wa Dar Es Salaam Young Africans Hans Van Der Pluijm anasisitiza kuwa kikosi chake kipo fiti na kina uwezo wa kuishangaza Al Ahly katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa katika uwanja wa Borg Al-Arab Stadium mjini Alexandria.

“tunaweza kushinda Nchini Misri japo haitakuwa rahisi, tunatakiwa kuwa makini na tayari kwa mchezo. Tutaanza kwa kulinda halafu baadae tushambulie ili tupate goli” aliema Kocha huyo mwenye umri wa miaka 66 kwa sasa.

“lakini lazima ifahamike kuwa tunaenda kucheza na timu bora zaidi barani Afrika. Ni mabingwa wa muda wote wa michunao hii ya Klabu Bingwa Afrika, kwahiyo unahitaji kufanya kazi ya ziada na maarifa zaidi kuweza kuwashinda” aliongeza Mdachi huyo ambae ameshawahi kuifundisha Berekum Chelsea ya Ghana na kufika hatua ya makundi mwaka 2012 ambapo walikutana na Al Ahly.

Historia haiwabebi Yanga hasa pale wanapocheza na Al Ahly kwani hawajawahi kushinda katika ardhi ya Misri na hawajaweza kuifunga Al Ahly takribani miaka nne iliyopita.

Beki wa kushoto wa Yanga Haji Mwinyi anasema kwamba wanajiandaa vyakutosha kuelekea mechi yao hiyo huku pia wakiwa wanaifuatilia Al Ahly kwa kuangalia mikanda ya mechi zao ili kuweza kubaini mapungufu yao.
“Naamini tunaweza tukawashinda katika ardhi yao ya nyumbani. Tumekuwa tukifanya mazoezi makali kuelekea mchezo huo tangu wikiendi iliyopita” alisema Mwinyi.

“kama tukiweza kupunguza mashambulizi yao, mchezo utakuwa rahisi kidogo kwetu. Mawinga wao ni wazuri sana na wanambinu za hali ya juu” aliongezea Mzazibar huyo mchezaji wa zamani wa KMKM.

Kaptaini wa timu hiyo Nadir Haroub maarufu kama “Cannavaro”  jina alilopewa baada ya kufananishwa uwezo wake na beki wa zamani wa Itali aliongezea kwa kusema “Tunapaswa kucheza kwa uangalifu na kwa nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kuwashinda. Naamini kocha wetu anambinu nzuri kuelekea mchezo huo na kama tukifuata maelekezo yake tunaweza tukawafunga”

0 comments:

Post a Comment