Friday, April 29, 2016

SIMON MIGNOLET HATARINI KUTIMULIWA LIVERPOOL


Mlinda mlango wa Liverpool  Simon Mignolet ameonekana kuwaangusha mamilioni ya mashabiki wa Liverpool msimu huu na kocha Klopp anafikiria kumleta kipa mwingine anayechezea Barcelona kwa sasa Marc-Andre ter Stegen.
Mlinda mlango huyo wa Barcelona anayesifiwa sana kwa kiwango chake alichoonyesha klabuni hapo tangu alipojiunga mwaka 2014, amekuwa katika mipango ya Jurgen Klopp ili kuimarisha kikosi chake katika nafasi hiyo ya mlinda mlango.


Alipoulizwa hivi karibuni kuwa yeye anafikiri ni kipa gani Louis Enrique atakuwa na mipango nae ya baadae, Ter Stegen alisema “Sijui kocha anachokifikiria” Comment ambayo imeongeza hisia kuwa huenda mlinda mlango huyo akawashiwa taa nyekundu klabuni hapo, kwani licha ya kufanya vizuri na kudhihirisha uwezo wake mkubwa klabuni hapo, Ter Stegen amecheza katika mechi 4 tu katika mechi zote za ligi msimu huu, huku Claudio Bravo akionekana kuwa ndo chaguo namba moja la Enrique. 






Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment