Friday, April 29, 2016

RUFAA YA MICHEL PLATINI KUTOLEWA MAAMUZI MAPEMA WIKI IJAYO


ALIYEKUWA Rais wa UEFA Michel Platini ameonekana mbele ya waandishi wa habari ijumaa hii katika mahakama inayojishugulikia usuluhishi wa masuala ya michezo, kupinga kifungo alichopewa cha miaka 6 ya kutojihusisha na masuala ya Mpira wa miguu akisema ana uhakika wa kushinda rufaa hiyo, Sepp Blatter rais wa Zamani wa Fifa akiwa miongoni mwa mashahidi wake.

Platini aliyeletwa na na taxi katika mahakama hiyo ya usuluhishi wa masuala ya michezo (Court of Arbitration for Sports-CAS) ana matumaini kuwa kifungo hicho alichokipata atakishinda kwa kushinda rufaa hiyo.
CAS imesema maamuzi ya rufaa ya Platini yanaweza kufanywa mapema sana mwa wiki ijayo kutegemeana na siku ambazo watakaa kuijadili rufaa hiyo.

“Leo, tupo katika mwanzo wa mchezo, mchezo mpya wa fainali, ni matumaini yangu kuwa matokea ya mchezo huu yatakuwa mazuri” alisema Platini ambae alipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Sepp Blatter kama Rais wa Fifa kabla ya kukumbana na kifungo hicho.

Platini alifungiwa kwa kipindi cha miaka 8 December mwaka jana pamoja na Blatter, kamati ya maadili ya Fifa ikihusika katika kutoa adhabu hizo. Wote wawili (Platini & Blatter) walikataa mashitaka yao na kupunguziwa adhabu kutoka miaka 8 hadi 6 baada ya kamati ya Fifa inayoshughulikia rufaa kupitia rufaa yao mwezi wa pili mwaka huu.

Blatter ambaye rufaa yake itasikilizwa siku chache zijazo, aliwasili mahakamani hapo saa 3 baadae na alipofuatwa azungumze alisema “Mimi ni shahidi katika kesi ya Mr. Platini leo na nitajibu maswali kama shahidi, asante kwa muda wenu”

Villar, Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Hispania (RFEF) aliwasiri na kisha kuondoka bila kujibu maswali aliyoulizwa. 


Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment