Friday, April 29, 2016

LIVERPOOL YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA VILLARREAL


KIKOSI Cha Liverpool chini ya kocha Mjerumani Jurgen Klopp kimeshindwa kuendeleza ubabe mbele ya klabu ya Villarreal kutoka nchini Hispania katika mechi ya kwanza ya Hatua ya Nusu fainali Europa League.
Klabu ya Villarreal ambayo imeshinda mechi zote za mashindao hayo msimu huu katika uwanja wa nyumbani huku wakiruhusu kufungwa mara moja tu katika dimba hilo la Estadio El Madrigal, ilipata ushindi huo baada ya goli lililofungwa dakika ya 92 ya mchezo goli lililofungwa na Adrian.
Liverpool sasa wanakuwa na kibarua kizito katika mechi ya marudio itakayocheza Anfield Nchini Uingereza.



WAFUNGAJI BORA WA LIGI HIYO HADI SASA

Aubameyang- Dortmund  11
Aduriz- Athletic Club        10
Reus-Dortmund                  9
Bakambu- Villarreal           9
Mak- PAOK                         9

MECHI NYINGINE ILIYOCHEZWA JANA

Shakhtar 2 - 2 Sevilla




Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment