Klabu ya Everton ipo tayari kukaa kikao leo na kujadili
hatima ya kocha wa timu hiyo Roberto Martinez.
Martinez amezungumza jana kuwa Bodi ya Everton iko sahihi
kujadili hatima yake kufuatia mwenendo mbovu wa timu hiyo.
Everton ambayo inacheza na Bournemouth wikiendi hii imekuwa
na msimu mbovu wakiwa wanashika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi. Kiwango kibovu
kinachoonyeshwa hasa katika uwanja wa nyumbani ndo limekuwa suala kubwa sana
ambalo linawaumiza mashabiki, wakiwa wameshinda michezo 4 tu katika uwanja wao
wa Goodison kitu ambacho kinamfanya Martinez kuwa katika wakati mgumu klabuni
hapo.
Martinez ambae alikuwa na misimu mizuri sana katika klabu za
Swansea City na Wigan Athletic kabla hajajiunga na Everton ni wazi kuwa
ataonyeshwa mlango wa kutokea na wamiliki wa timu hiyo Farhad Moshiri na
mwenyekiti Bill Kenwright sambamba na jopo zima la bodi ya timu hiyo kufuatia
kiwango kibovu cha timu hiyo iliyochini ya Mhispania huyo mwenye umri wa miaka
42.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment