Beki wa Liverpool amekataa kuchukuliwa vipimo kwa mara ya
pili baada ya majibu ya vipimo vya kwanza kuonyesha alikuwa anatumia dawa za
kupunguza unene ambazo haziruhusiwi kwa wanamichezo. Kukataa huko kumelifanya
shirikisho la Mpira barani ulaya UEFA kumfungia mchezaji huyo kwa muda wa siku
30.
UEFA wamesema katika tovuti yao kuwa “hatua za kinidhamu
zitachukuliwa dhidi ya Mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho kufuatia vipimo
vilivyofanyika katika mechi ya UEFA Europa League raundi ya 16, katika mchezo
wa pili kati ya Mancester United na Liverpool
iliyochezwa March 17 mwaka huu”.
UEFA wamesisitiza kuwa hatua zaidi za kinidhamu
zitachukuliwa dhidi ya mchezaji huyo hasa baada ya kukataa kufanyiwa vipimo kwa
mara ya pili.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment