Thursday, April 28, 2016

Guardiola Aendeleza Rekodi Mbaya Mechi Za Ugenini



KOCHA wa Bayern Muchen Pep Guardiola jana ameshuhudia vijana wake wakishindwa kutamba mbele ya Atletico Madrid iliyo chini ya Diego Simeone. Mechi hiyo ya kwanza ya Nusu fainali Klabu bingwa Ulaya ilizikutanisha Atletico na Bayern katika uwanja wa Vicente Calderon Nchini Hispania. Hii inakuwa ni mechi ya 8 mfululizo Guardiola kushindwa kupata ushindi Ugenini. 


Bayern ilikubali kichapo cha goli 1 - 0 kutoka kwa Atletico goli lililofungwa na Saul dakia ya 11. Bayern wanalazimika kupata magoli mawili kwa bila ili waweze kutinga katika hatua ya fainali.


Guardiola pia atakuwa na hofu na kiwango cha  mshambuliaji wake hatari Lewandowski ambae hajafunga goli katika michezo 8 kati ya tisa waliyocheza ugenini.


Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment