kocha huyo wa Bayern Muchen amemwomba msamaha mshambuliaji huyo wa Ureno na Klabu ya Real Madrid Christiano Ronaldo kufuatia kile alichokiita Guardiola kuzima ndoto za Ronaldo nusu Fainali ya UEFA Champions.
Bayern iliwaondosha Benfica katika hatua ya robo fainali baada ya sare ya 2 - 2 iliyoipata Bayern ikiwa ugenini.
Kabla ya mechi hiyo kati ya Benfica na Bayern Muchen Christiano Ronaldo alinukuliwa akisema anaamini atakutana na klabu ya Benfica katika hatua ya nusu faili. CR7 aliyasema hayo akiamini kuwa Benfica wangeweza kuindosha Bayern klabu inayonolewa na Guardiola.
Baada ya Bayern kuisambaratisha Benfica Guardiola alitoa salamu za pole kwa Christiano Ronaldo kufuatia timu yake hiyo aliyokaipa nafasi ya kuiondosha Bayern kuondolewa katika michuano hiyo.
"Najua Ronaldo alitamani sana kukutana na Benfica katika hatua ya nusu fainali, hivyo nampa pole kwa hilo" alisema Guardiola
0 comments:
Post a Comment