Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" inashuka dimbani tena leo Mei 21 kucheza na Malaysia.
Serengeti Boys inayofanya vizuri katika michuanao hiyo huko nchini India ilifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kutoka sare ya 2 - 2 na Korea Kusini katika mfululizo wa michuano hiyo maalumu ya kimataifa ililyoandaliwa na Shirikisho la soka nchini India (AIF Youth 2016-U-16) na leo itashuka tena dimbani kucheza na Malaysia katika mchezo wa mwisho wa kundi na endapo Serengeti Boys watashinda katika mchezo huo basi watatinga moja kwa moja katika hatua ya Fainali.
Serengeti Boys mpaka sasa imeshacheza mechi 3 na kuifunga India 3-1 na kutoka Sare na USA 1-1 na kisha South Korea 1-1.
Ili kutinga Fainali Serengeti Boys wanapaswa kuifunga Malaysia ambayo imetoka sare na India na kubondwa na South Korea 3-0.
Ikiwa Serengeti Boys wataifunga Malaysia basi njia yao itakuwa nyeupe ikiwa pia mechi kati ya Marekani na Korea Kusini itaisha kwa timu moja kushinda
Akizungumzia mchezo huo kocha wa Timu hiyo Bakari Shime amesema kikosi kiko vizuri na wamejiandaa kukabiliana na mchezo huo huku akikiri kuwa mchezo utakuwa mgumu na hivyo wanahitaji kupambana ili kuweza kupita katika hatua hiyo.
Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25, 2016 na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja wa Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India.
India imeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SERENGETI BOYS
0 comments:
Post a Comment