West Bromwich Albion imezima ndoto za Spurs baada kuwalazimisha sare ya goli 1 - 1. Spurs walikuwa wakwanza kupata goli kipindi cha kwanza cha mchezo dakika ya 33, goli la kujifunga la Dawson. Hadi timu zinaenda mapumziko Tottenhama walikuwa mbele kwa goli 1 - 0. West Bromwich hawakukata tamaa wakaendelea kupambana na hatimaye dakika ya 73 Dawson yule yule ambae alijifunga goli dakika ya 33 alirekebisha makosa yake na kuifungia timu yake goli la kusawazisha. Hadi mpira unaisha Tottenham 1 - 1 West Bromwich.
Matokea haya yamepeleka furaha kubwa kwa klabu ya Leicester City kwani sasa hivi wanatakiwa kushinda mechi moja tu kwa maana ya kupata pointi 3 tu ili kutangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu. Leicester wana pointi 76 huku Tottenhama wakiwa na pointi 69 wote wakiwa wamecheza michezo 35, hivyo tofauti ya pointi inakuwa ni pointi 7 zikiwa zimebaki mechi 3 tu kumaliza ligi, hivyo Leicester wakishinda mechi moja tu kati ya mechi zao tatu zilizobaki watafikisha pointi 79 wakati Tottenham wakishinda mechi zote tatu watafikisha pointi 78 na kuifanya Leicester kuwa mbele kwa pointi 1.
Mechi za Leicester zilizobaki ni dhidi ya Manchester United, Everton na Chelsea, wakati Tottenham wao wamebakiza mechi dhidi ya Chelsea, Southampton na Newcastle United.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment