Uongozi wa klabu ya Liverpool unaamini uwepo wa Jurgen Klopp klabuni hapo huenda ukaamua hatima ya Mario Gotze Msimu ujao. Gotze anaeonekana kuto kupata nafasi kwa sasa katika klabu ya Bayern anawindwa huenda akaondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Liverpool na Borussia Dortmund watapambana katika kuinasa saini ya mchezaji huyo.p. Liverpool wanaonekana kumhitaji mchezaji huyo ambae amewahi kutwaa kombe la dunia akiwa na Timu yake ya Taifa ya Ujerumani mwaka juzi lakini Dortmund nao wamethibitisha kumuhitaji mchezaji wao huyo wa zamani.
Gotzea alijiunga na Bayern mwaka 2013 akitokea Dortmund kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 32. Kuondoka kwake kuliwaudhi sana mashabiki wa Dortmund kwani alitoa kauli ya kutaka kujiunga na Bayern siku chake kabla ya mechi yao ya nusu fainali ya UEFA dhidi ya Real Madrid. Wiki mbili baadae Dortmund na Bayern zilikutana katika fainali ya UEFA Champions League katika uwanja wa Wembly, fainali ambayo Gotze aliikosa kutokana na kuwa majeruhi.
Mtendaji Mkuu wa Dortmund Hans-Joachim Watzke amethibitisha kuwa klabu inamuhitaji Gotze lakini atatakiwa kutoa maelezo ya kwanini aliondoka klabuni hapo.
Akiongea na waandishi wa habari Watzke alisema “Kama yupo sokoni (Gotze), ni wazi kuwa tutakaa kumjadili, Mlango uko wazi kwa mchezaji yoyote anehitaji kujiunga na Dortmund”.
Mabango yametandazwa na mashabiki katika uwanja wa Dortmund yanayoashiria kumdharau Gotze, lakini Watzke anaamini mashabiki wanaweza kutulizwa na kusahau yaliyopita na kumpa nafasi nyingine Gotze.
Watzke Aliongeza kwa kusema “kama akirudi Dortmund, tutazungumza na mashabiki na Gotze atatakiwa kuwaambia mashabiki ni kwanini aliondoka klabuni hapo na kujiunga na Bayern”
Upande wa pili Klopp anamuona Gotze kuwa ndo kipaumbele chake cha kwanza katika msimu ujao wa usajili.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment