KOCHA mpya wa Chelsea Antonio Conte licha ya kuwa anapenda
kuwaacha mastaa wake wote katika kikosi hicho na alishaitisha kikao na timu
kuliweka wazi suala hilo, amekubali kuwa licha ya kukosa nafasi ya kucheza
klabu bingwa ulaya atapambana kuhakikisha anabakisha mastaa wake wote klabuni
hapo.
Kufuatia kuondoka kwa John Terry wachezaji wengine ambao nao wapo mbioni kuondoka klabuni hapo ni pamoja na Eden Hazard, Diego Costa, Willian na
Thibaut Courtois.
Conte amekubali kuwa mlinda mlango Thibaut Courtois anaweza
kuuzwa kwa dau la paundi milioni 50. Courtois aliyekachukua nafasi ya Peter
Cech akitokea Atletico Madrid alikokicheza kwa mkopo ameonekana kutoridhishwa
vizuri na maisha ya hapo Stamford Bridge. Miongoni mwa sababu ambazo zinamtoa
Courtois klabuni hapo ni pamoja na Chelsea kushindwa kuingia katika nafasi 4 bora ambazo zingewawezesha kushiriki mashindano ya UEFA Champions League msimu ujao.
Paris Saint-Germain na Real Madrid wako tayari kumchukua mlinda
mlango huyo na inaonekana klabu hizo zote mbili zina uwezo wa kutoa kitita
hicho cha pesa. Kuhusu nani atachukua nafasi yake, Mlinda mlango wa Southampton
Fraser Forster anatajwa kujiunga na klabu hiyo ya Chelsea.
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
Pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment