Tuesday, November 8, 2016

Huzuni yatanda Tanzania baada kuondokewa na Mzee Said Mohamed Abeid


Majonzi yametawala katika nyuso za wapenda soka nchini baada ya kuondokewa na Mzee Said Mohamed Abeid ambae ni mwenyekiti wa timu ya Azam pia ni makamu mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu Tanzania bara na mjumbe wa kamati mbalimbali za shirikisho la soka Tanzania, TFF.
Mpaka umauti unamkuta alasir ya jana Novemba 7, 2016, na Mzee Said Mohamed Abeid alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam.
Huko shinyanga ambapo timu ya Azam imekwenda kumalizia mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui FC hali ya huzuni imetanda sana Miongoni mwa wachezaji, benchi la ufundi, na viongozi wote walioambata na timu hiyo
Mzee Said atakumbukwa Kutokana na mchango wake mkubwa katika kilabu ya Azam tangu kupanda daraja miaka 8 iliyopita, chini ya uongozi wake Azam imeweza kutwaa makombe mbalimbali ikiwemo ligi kuu Tanzania Bara, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, mapinduzi cup.
Mzee Saidi atakumbukwa kwa uchesi,upendo, ukarimu na uchapakazi wake katika soka la Tanzania.
Marehem alizaliwa visiwani Zanzibar mnamo tarehe 20 Machi 1940, amezikwa leo Jumanne ya tarehe 8 Novemba, 2016 kwenye makaburi ya Kisutu baada ya swala ya saa kumi (Alasir).

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee Said Mohamed Abeid mahali pema peponi amiin

0 comments:

Post a Comment