Thursday, July 7, 2016

YANGA SASA KUKIONA CHA MOTO

Klabu ya Yanga ipo hatarini kuburuzwa katika mahakama ya kibiashara na wadhamini wao kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Yanga Huenda ikafikishwa mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuvunja mkataba na wadhamini wao kampuni ya TBL.

Habari zaidi zinasema TBL inakusudia kuipeleka Yanga Mahakaman kutokana na kushindwa kutimiza makubaliano ya mkataba wao.

"Hatua ya makundi ambayo Yanga wamefika ilikuwa ni muhimu sana kwa mdhamini wao kumtangaza, lakini badala yake wameingia hatua hiyo wameondoa nembo ya mdhamini wao , wakati bado wapo ndani ya mkataba, hivyo TBL inapanga kuipeleka Yanga katika mahakama ya Biashara, mwezi mmoja uliobaki ulikuwa na manufaa zaidi kwa wadhamini na maana kubwa kuliko kipindi chote ambacho wamewadhamini" alisema Ofisa kutoka katika kampuni hiyo ya TBL.

Ofisa huyo aliongeza kuwa kinachoshangaza zaidi ni kwamba Yanga wameenda Algeria wameondoa nembo ya mdhamini kifuani, na kwamba siku za hivi karibuni wamekuwa na maelewano ambayo sio mazuri na mdhamini huyo.

Hata hivyo Yanga haijatangaza rasmi kuvunja mkataba na TBL lakini tayari wameanza kuutumia mkataba wa Quality Group Limited inayomilikiwa na Yusuf Manji mwenyekiti wa klabu hiyo.

Aidha Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji kupitia tarifa yake ya hivi karibuni amesema kuwa mkataba wa Yanga na TBL uliosainiwa miaka mitano iliyopita na mtangulizi wake (Mwenyekiti aliyepita) ulikuwa ni haramu, kwani mamlaka ya kutia saini kwa mujibu wa katiba ya Yanga yapo kwa bodi ya wadhamini.
Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook



0 comments:

Post a Comment