Monday, April 25, 2016

Simba Yaendelea Kujifua Huko Visiwani Zanzibar



Timu ya Simba Sports Club imeendelea na mazoezi tena leo huko visiwani Zanzibar yakiwa ni maandalizi dhidi ya mchezo wao na Azam FC.
Simba ambao kwa mechi za hivi karibuni wamekuwa hawafanyi vizuri wameelekea visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo huo muhimu zaidi kwao kwani msimamo wa ligi bado unawapa nafasi ya kupigania ubingwa wa ligi kuu Bara Msimu huu. Kwa takribani miaka mitatu sasa hivi Simba hawajashiriki mashindano ya kimataifa kitu ambacho kinawanyima usingizi sio tu viongozi wa klabu hiyo bali pia Mashabiki na wapenzi wa Simba wanaumia kuona timu yao inakosa kushiriki michuano ya Kimataifa.

Simba wanahitaji ushindi ili kuongeza presha kwa Yanga wanaoshika nafasi ya kwanza katika msimamo huo wakiwa wamewaacha Simba kwa pointi mbili tu. Msimamo wa ligi jinsi ulivyo timu yoyote kati ya Simba, Yanga na Azam FC inaweza kuibuka bingwa wa Msimu huu kwani timu hizi zinatofautina kwa pointi chache sana.

Kutokana na kuanzishwa kwa kombe la shirikisho (FA) timu itakayochukua nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu haitashiriki katika mashindano ya kimataifa kama ambavyo ilikuwa inafanywa hapo mwanzo badala yake mshindi wa kombe la FA ndiye atakaeshiriki mashindano ya kimataifa pamoja na mshindi wa ligi kuu Bara. Simba iliondoshwa katika michuano ya FA wiki moja iliyopita baada ya kukubali kipigo cha goli 1 - 0 kutoka kwa Coastal Union mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa hivyo kuifanya Simba kuelekeza nguvu zao zote katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambako wananafasi ya kuchukua ubingwa endapo watafanya vizuri katika mechi zao zote zilizobaki huku wakiwaombea wapinzani wao kupoteza japo mechi moja huku wao wakishinda mechi zote ambapo watamaliza ligi wakiwa mbele kwa tofauti ya pointi moja.

Simba wanahitaji utulivu na kuondosha tofauti katika klabu yao na kuongeza hamasa kwa wachezaji ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuibuka mabingwa.









pata habari za michezo kwa haraka zaidi kupitia soka24.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment