Wednesday, November 9, 2016

Azamu yamuenzi Mzee Said Mohamed Abeid kwa ushindi, Simba yaangukia pua Mbeya


Huko Mbeya wakicheza kwa tahadhari kubwa huku wakikumbuka vipigo viwili mfululizo walivyopata katika mechi zilizopita, timu ya Tanzania Prisons imeadhibu simba goli 2 – 1 katika mechi ya kukamilisha raundi ya kwanza.
Mchezo ulianza kwa simba kuliandama lango la wenyeji wao huku tukimshudia Mavugo, na Mnyate wakipoteza nafasi za wazi ambazo zingeipatia simba uongozi mapema, iliwachukua simba dakika 43 kujipatia goli kupitia kwa Mnyate baada ya kuunganisha kwa kichwa pasi safi ya Kichuya.
Kipindi cha pili Tanzania Prisons waligeuza aina ya mchezo na kuwazua simba kupiga krosi huku wakishambulia kwa kushtukiza na mnamo dakika ya 47’ na 64’ kupitia kwa Hangayaa .
Hadi mwisho wa mchezo huo Tanzania Prisons 2 simba 1.

Shinyanga mambo yamewaendea vizuri Azam Fc baada ya kupata ushindi wa kwanza mkubwa katika msimu huu baada ya kuitandika bila huruma timu ya Mwadui kwa magoli 4 – 1.
Mwadui ndio waliotangulia kuliona lango la Azam dakika ya 30 kupitia kwa Hassan Kabunda, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Mwadui 1 Azam 0.

Kipindi cha pili 54’ John Bocco aliisawazishia Azam, dakika ya 71 Shaaban Idd alifunga goli la pili dakika 74 Shaaban Idd alifunga la tatu na alifunga tena la nne na la tatu kwake.

0 comments:

Post a Comment