Saturday, October 29, 2016

Azam yaishusha mtibwa yainyatia stand utd, michezo mitano kupigwa leo


Baada ya jana ijumaa timu ya azam kuibuka na ushindi ugenini wa goli 3 – 2 dhidi ya wenyeji wao Kagera sugar na kufufua matumain ya kuwania kombe la Vodacom baada ya kufikisha pointi19 nyuma ya stand utd, Yanga na simba.
Leo jumamosi na kesho jumapili ligi hiyo itaendelea katika nyasi za viwanja mbalimbali kama ifuatavyo
Huko jijini Mbeya wenyeji Mbeya City wataikaribisha timu inayokuja kwa kasi kutoka chini baada ya kubadili kocha na kumrudisha Kali Ongala Majimaji ya Songea katika dimba la Sokoine.
Mchezo mwingine ni kati ya wenyeji Toto Africans dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika dimba la CCM Kirumba.
Mchezo unaosubiriwa kwa hamu ni kati ya vinara wa ligi hiyo Simba watakapokuwa wageni wa timu ya Mwadui FC ya Shyinyanga, katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Africans Lyon itakua mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye uwanja wa Uhuru,
Mchezo wa mwisho siku ya leo ni kati ya JKT Ruvu ya Pwani na Ndanda FC ya mkoani Mtwara katika dimba la Mabatini mkoani Pwani.

Kesho jumapili Mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakiwa na furaha baada ya kurudi kwa kocha wao mkuu watashuka uwanja wa Uhuru kuikaribisha timu iliyopanda daraja kutoka Mwanza timu ya Mbao FC, Wakati huko Mkoani Pwani wenyeji Ruvu Shooting Star itakapoikaribisha timu yaStand United ya Shinyanga.

0 comments:

Post a Comment