Sunday, October 16, 2016

RATIBA LIGI KUU BARA LEO JUMAPILI


Michezo kadhaa kupigwa jumapili hii kote duniani tukianzia nyumbani Tanzania ligi kuu Tanzania Bara kuendelea katika viwanja vinne vya miji tofauti.
Macho ya wapenda michezo wengi Afrika mashariki yapo uwanja wa Uhuru ambapo utafanyika mchezo namba 76 utakao zikutanisha Azam matajiri hawa wa jiji na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga, ikumbukwe kua Yanga na Azam  wanapokutana Hakuna kuoneana haya kwani hua huwezi kutabiri ni nani ataibuka mshindi wa mchezo. Mchezo huo wa leo jioni majira ya saa kumi utachezeshwa na mwamuzi  Israel Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo atasaidiwa na Soud Lila na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar es Salaam.
Mchezo mwingine ni mchezo namba 77 utakaopigwa dimba la Mabatini Mlandizi Pwani wakati wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani zidi ya timu ya jiji la Mbeya Mbeya city mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi  Rudovic Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jeremina Simon wa Dar es Salaam.Kamisha wa mchezo huo atakuwa Idelfonce Magali wa Morogoro.
Mchezo mwingine utazikutanisha Mtibwa sugar ambayo inakumbukumbu ya kipigo cha goli 3 kwa 1 kutoka kwa Yanga katikati ya wiki wataikaribisha Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo namba 78 ambao utachezeshwa na mwamuzi  Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi ni Ferdinand Chacha wa Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa akiba Nicolaus Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa Dodoma.
Mchezo mwingine ni ule wenye namba 78 kati ya wenyeji wa mkoa wa mwanzaToto African ya Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mchezo huo utasimamiwa na mwamuzi Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa Mwanza. Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar es Salaam.
Ratiba hii ni kwa msaada wa Tff
Michezo yote itapigwa saa kumi kamili jioni





0 comments:

Post a Comment