Saturday, October 15, 2016

MATOKEO YA MICHEZO YA EPL LEO JUMAMOSI


Ligi kuu ya uingereza imeendelea tena leo kwa michezo sita kupigwa katika viwanja sita tofauti
Mchezo wa mapema ulipigwa Stamford bridge pale Chelsea walipoiadhibu bila huruma bingwa mtetezi wa ligi hiyo Leicester City kwa goli 3 bila majibu kwa  magoli ya Diego costa dakika ya 7 kabla ya Eden Harzad kufunga la pili dakika ya 33 na msumari wa mwisho ulipigiliwa na mnigeria Victor Mosses dakika ya 80 na kuifanya Chelsea kufikisha alama 16 na kupanda mpaka nafasi ya 5
Wakati huohuo mambo yanaendelea kumuendea kombo Gudiola baada ya leo kukaliwa kooni na kulazimishwa kutoka sare ya goli 1 kwa 1 na Everton, ilikua ni Everton ndio walioanza kulifumania lango la Man city dk 64 kupitia kwa Lukaku kabla ya Nolito kuisawazishia city katika dk 72
Stoke city wao walitoa onyo kwa sunderland kwa kuibugiza magoli miwili kwa bila kwa magoli ya Joe Allen dk 9 na 45 ya mchezo
Arsenal wameendelea kutoa dozi na kuikaribia man city kileleni baada ya kuipiga kumbo Swansea city 3 2 kwa magoli miwili ya Theo Walcot na moja la Mesut Ozil magoli ya Swansea yalifungwa na Sigurdsson na Borjan Boston
AFC Bournemouth imefanya kufuru  kwa Hully City baada ya kupiga goli 6 kwa  1

West Bromwich Albion wameondoa furaha ya Tottenham Hotspur waliyokua nayo wiki moja iliyopita baada ya kuifunga man city baada ya kugawana alama mojamoja Kutokana na sare ya 1 1 goli la Tottenham Hotspur likifungwa na Dele Alli dk 89 huku lile la mapema la West Bromwich Albion likifungwa dk44 James mc Clean


0 comments:

Post a Comment