Wednesday, April 6, 2016

WAKATI SIMBA WAKIMWANDIKIA BARUA, KIIZA AREJEA KIMYA KIMYA

Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza ametua jijini Dar es Salaam kimyakimya ikiwa ni saa chache baada ya uongozi wa Simba kuandika barua ukimtaka kujieleza.

KIIZA- WATATU KULIA AKIWASILI NCHINI
Uongozi wa Simba umetangaza kuchukua uamuzi huo baada ya Kiiza mwenye mabao 19 ya Ligi Kuu Bara na beki Juuko Murshid kuchelewa kurejea nchini kwa siku sita wakitokea kwao nchini Uganda.

Wakati uamuzi huo umetangazwa, Kiiza ameonekana akiranda katika mitaa ya jijini la Dar es Salaam.

Moja ya maeneo aliyoonekana ni Mlimani City akionyesha yuko tayari na kujiunga na kikosi cha Simba.


Hata hivyo, bado haijajulikana kama Kiiza atajibu lini barua hiyo ya kutakiwa kutoa maelezo kabla ya kuchukuliwa hatua au kujisahau.

Related Posts:

  • OMOG ASHUSHA PRESHA ZA WANAMSIMBAZI Kocha wa klabu ya Simba, Mcameroon, Joseph Omog amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kufuatia sare ya bila kufungana waliyoipata dhidi ya JKT Ruvu. Omog amesema hayo ni matokeo ya kawaida ya kimchezo hivyo mash… Read More
  • PLUIJM:"YANGA TIMU BORA TANZANIA" Kocha wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Hans Van Pluijm amesema Yanga bado ni timu bora zaidi Tanzania Licha ya kuondolewa katika michuano ya kimataifa. Yanga imetupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho … Read More
  • SIMBA YABADILI GIA ANGANI Sare ya bila kufunguna waliyoipata Simba dhidi ya JKT Ruvu imemfanya kocha wa klabu hiyo, Joseph Omog kubadili mfumo wa uchezaji na kusisitiza umakini kwa wachezaji katika mechi zijazo. Katika mchezo huo dhidi ya JKT Ruvu… Read More
  • BOCCO AITISHIA NYAU SIMBA ZIKIWA zimesalia siku tatu kabla ya kupambana na Simba, Nahodha wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, amesema kuwa wanamorali kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo utakaofanyika … Read More
  • TANZIA;BABA YAKE DEOGRATIUS MUNISH "DIDA" AAGA DUNIABaba wa Mlinda Mlango namba 1 wa Mabingwa Watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, Deogratius Munish amefariki Dunia mchana wa leo. Mzee Munishi ameaga dunia mchana wa leo, kifo chake kimetokea wakati tayari Dida anakaribia kuingi… Read More

0 comments:

Post a Comment