Mbunge wa Tandahimba kupitia Chama cha Wananchi (Cuf), Katani Ahmad Katani ametoa kitita cha Sh 500,000 kwa wachezaji wa Ndanda FC baada ya kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam FC, leo.
Ndanda FC imeonyesha si laini baada ya kuilazimisha sare ya mabao 2-2 Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Katani amesema amefurahishwa na Ndanda na pia kuahidi kutoa Sh milioni moja kwa kila mechi ambayo Ndanda watashinda.
“Pia nitanunua kila bao watakalofunga kwenye mechi zao, Ndanda ni timu ya mkoa wa Mtwara ambako ninatokea.
Ninafanya hivi kuwahamasisha vijana ili wapambane zaidi,” alisema Katani.
Ndanda ilionyesha soka la kuvutia katika kipindi cha pili wakati wa mechi yao dhidi ya Azam FC leo na kusawazisha mabao yote mawili baada ya wenyeji wao kutangulia kwa kuwafunga mabao mawili.
Wednesday, April 6, 2016
NDANDA FC WAMIMINIWA MIPESA BAADA YA SARE NA AZAM FC
Related Posts:
"Nisipompanga Cannavaro, Basi Nitampanga Mwingine Mwenye Uwezo" Kauli Ya Hans Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema nahodha na beki wake wa kati wa timu yake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ yupo fiti kucheza mechi ya leo dhidi ya Al Ahly ila ni siri yake kuhusu kucheza. Cannavaro ni kati ya wachezaji… Read More
Yanga Na Azam Kuipa TFF Mamilioni Ya Pesa Achana na klabu zenyewe kuneemeka, Azam FC na Yanga zikifuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho basi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litapata fedha kutokana ushiriki wa timu hizo. Yanga ipo katika Ligi ya M… Read More
Ndanda Kosovo Afariki Dunia Ndanda Kosovo Enzi Za Uhai Wake Mwananamuziki maarufu wa dansi nchini, Ndanda Kosovo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Taarifa zinazotufikia, zinaeleza Ndanda amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo. … Read More
Mgomo Wa Yanga Dhidi Ya Al Ahly Kuelekea Mechi Yao Leo Manji Rais Wa Yanga Uongozi wa Dar Young Africans umegoma kuwauzia wapinzani wao, Al Ahly ya Misri haki za kurusha matangazo ya mechi baina yao Mechi itakayochezwa Leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ndo wenyeji wa m… Read More
First Eleven Ya Yanga Hii Hapa Leo Dhidi Ya Al Ahly KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA DHIDI YA AL AHLY LEO, HIKI HAPA… 1. Ally Mustapha 2. Juma Abdul 3. Mwinyi Haji 4. Kelvin Yondani 5. Vicent Bossou 6. Thabani Kamusoko 7. Deus Kaseke 8. Salum Telela 9. Amissi Tambwe 10. Donald N… Read More
0 comments:
Post a Comment