
LIGI Kuu Tanzania Bara imeendelea tena hivi leo katika viwanja 4, huko Jijini Mwanza wenyeji Toto Africans Wakiikaribisha Yanga. Mchezo huo ulioshuhudiwa na maelfu ya watazamaji ulikuwa na wa kuvutia ukizingatia kwamba timu hizo mbili licha ya kuhusishwa na undugu leo ziliingia uwanjani kila moja ikihitaji ushindi katika mchezo huo.
Toto ndo walikuwa wa kwanza kupata goli kipindi cha kwanza cha mchezo dakika ya 39 goli lililofungwa na William...